Raia wa Afrika Kusini wapiga kura kwenye uchaguzi mkuu (4)
![]() |
Mwanamke akipiga kura kwenye kituo cha kupigia kura huko Soweto, Johannesburg, Afrika Kusini, Mei 29, 2024. (Picha na Shiraaz Mohamed/Xinhua) |
JOHANNESBURG - Waafrika Kusini wamepiga kura siku ya Jumatano asubuhi kwenye uchaguzi mkuu wa Mwaka 2024 nchini humo ambapo wapiga kura zaidi ya milioni 27 walikuwa wakitarajiwa kupiga kura kwenye vituo zaidi ya 23,000 nchini kote kuchagua Bunge jipya la Kitaifa na majumbe wa mabaraza ya majimbo, kwa mujibu wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Afrika Kusini (IEC).
Uchaguzi huo wa kitaifa na majimbo wa Mwaka 2024 unaoambatana na maadhimisho ya miaka 30 ya uhuru na demokrasia nchini Afrika Kusini, ni uchaguzi mkuu wa saba kufanyika nchini humo tangu siasa za ubaguzi wa rangi kumalizika Mwaka 1994.
IEC imesema matokeo ya uchaguzi yatatangazwa Jumapili. Kisha Bunge jipya litamchagua rais mpya wa Afrika Kusini kwa miaka mitano ijayo.
Bunge hilo lina wajumbe 400. Jumla ya wajumbe 200 watachaguliwa kutoka kwenye orodha za vyama za kitaifa, wakati wengine 200 watachaguliwa kutoka kwenye orodha za vyama za majimbo tisa.
Kwa mujibu wa IEC, vyama 70 vya kisiasa na wagombea huru 11 wanashiriki katika uchaguzi huo wa mwaka huu. Wagombea huru wanashiriki katika uchaguzi huo kwa mara ya kwanza, huku majina yao yakionekana kwenye karatasi za kupigia kura kufuatia marekebisho ya sheria ya uchaguzi.
Zoezi la kuhesabu kura lilikuwa limepangwa kuanza saa 12 jioni siku ya Jumatano baada ya zoezi la kupiga kura kufungwa, huku matokeo yakipangwa kuanza kutolewa saa 12 alfajiri (0400 GMT) leo Alhamisi. Huku idadi ya wapiga kura inatarajiwa kuwa kubwa kutokana na hali ya hewa iliyotabiriwa kuwa nzuri kote nchini, zoezi la kuhesabu kura litachukua siku kadhaa kabla ya kukamilishwa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma