99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Uganda yasema dawa?za malaria zilizotolewa na China yanachangia kuzuia maambukizi (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 07, 2024
Uganda yasema dawa?za malaria zilizotolewa na China yanachangia kuzuia maambukizi
Waziri wa Afya wa Uganda Jane Ruth Aceng akizungumza kwenye hafla ya kukabidhiwa dawa za malaria zilizotolewa na China katika Duka la Dawa la Kitaifa huko Kajjansi, Wakiso, Uganda, Aprili 5, 2024. (Picha na Hajarah Nalwadda/Xinhua)

Uganda imesema dawa za kupambana na malaria zenye thamani ya dola za Marekani milioni 1.1 zilizotolewa na China zitasaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa maambukizi ya malaria katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Waziri wa Afya wa Uganda Jane Ruth Aceng alisema mwaka jana wagonjwa wa malaria waliongezeka sana nchini Uganda, ugonjwa ambao ulienea kwa zaidi ya nusu ya maeneo nchini humo.

Aceng alikuwa amezungumza Ijumaa baada ya kupokea dawa kutoka kwa Balozi wa China nchini Uganda, Zhang Lizhong, katika Duka la Dawa la Kitaifa la Kajjansi, eneo la katikati ya Wakiso.

“Kwa hiyo, msaada huu mkubwa wa dawa za malaria utasaidia katika mapambano dhidi ya malaria na kudhibiti maambukizi ya malaria hasa katika maeneo yenye hatari ,” alisema waziri huyo.

Balozi Zhang alisema ushirikiano katika nyanja ya afya ni moja ya sekta muhimu za ushirikiano katika uhusiano wa nchi hizo mbili.

"Msaada huo pia ni mradi wa matibabu na afya katika Mipango Tisa zilizoanzishwa kwenye Mkutano wa Nane wa Mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC)," Zhang alisema.

Tangu mwaka 1983, China imetuma timu 23 za madaktari wa China wapatao 218 nchini Uganda. Mamia kwa maelfu ya Waganda wametibiwa magonjwa mbalimbali.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha