99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Mbio za Marathon za Hohhot 2023 zafanyika kwa kishindo Hohhot, China (9)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 10, 2023
Mbio za Marathon za Hohhot 2023 zafanyika kwa kishindo Hohhot, China
Picha hii iliyopigwa na droni ikionesha uwanja wa Bustani ya Utamaduni wa Njia ya Hariri kwenye mbuga. (Picha ilitolewa na waandalizi)

Tarehe 9, Julai saa 1:30 asubuhi, mbio za marathon za Hohhot 2023 zilianza na kufanyika kwenye Bustani ya Utamaduni wa Njia ya Hariri kwenye mbuga ya eneo la Saihan la Mji wa Hohhot, Mkoa unaojiendesha la Mongolia ya Ndani nchini China.

Wanariadha na mashabiki wa mbio za marathon zaidi ya 15,000 kutoka ndani na nje ya China walikusanyika huko Hohhot, ili kushiriki na kushuhudia pamoja msimu wa michezo katika mji huo unaosifiwa kuwa “mji wa kijani” nje ya Ukuta Mkuu wa China.

Mbio hizo zimefanyika chini ya kauli mbiu ya “Kukutana tena Mji wa Mbuga, kufanya mbio za Marathon katika Mji wa kijani”, na zimeandaliwa na serikali ya Mji wa Hohhot.

Baada ya mashindano makali, mwanariadha Yang Dinghong kutoka Mkoa wa Yunnan wa China alishinda ubingwa wa mbio za marathon nzima kwa wanaume baada ya kumaliza mbio hizo kwa kutumia muda wa saa 2 dakika 19 na sekunde 46, na mwanariadha Cao Fengying kutoka Mkoa wa Hebei wa China alishinda ubingwa wa mbio za Marathon nzima kwa wanawake baada ya kumaliza mbio kwa kutumia saa 2 dakika 56 na sekunde 5.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha