99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Kenya kufanyia marekebisho bajeti baada ya kuondolewa kwa muswada wa fedha bungeni

(CRI Online) Julai 05, 2024

Rais wa Kenya, William Ruto amesema, serikali yake inafanyia marekebisho bajeti yake baada ya kuondolewa kwa Muswada wa Fedha 2024 bungeni, ambao umesababisha maandamano makubwa nchini humo katika wiki tatu zilizopita.

Rais Ruto aliyeongoza mkutano wa Baraza la Mawaziri jijini Nairobi hapo jana Alhamisi, amesema Hazina Kuu ya nchi hiyo itapunguza ukubwa wa bajeti ili kuleta uwiano kati ya mambo yanayopaswa kutekelezwa na yanayoweza kusubiri, na kuhakikisha kuwa miradi ya kitaifa haitaathiriwa.

Juni 13, Kenya iliwasilisha bajeti yake ya dola za kimarekani bilioni 30 kwa mwaka wa fedha 2024/2025, iliyolenga kudumisha ukuaji wa uchumi unaotarajiwa kufikia asilimia 5.5 mwaka huu.

Muswada wa Fedha wa mwaka 2024 uliosababisha maandamano nchini humo, ulitaka kuongeza dola za kimarekani bilioni 2.67 kupitia kodi mpya mbalimbali zilizopendekezwa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha