99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Tanzania yaiagiza TRA kutatua mgomo wa wenye maduka uliotokana na machafuko ya mrundikano wa kodi

(CRI Online) Juni 28, 2024

Serikali ya Tanzania Alhamisi iliiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ichukue hatua ili kukomesha mgomo wa siku nne uliofanywa na wenye maduka katika mikoa zaidi ya minane nchini humo.

Kwenye mkutano na wanahabari uliofanyika huko Dodoma msemaji mkuu wa serikali Thobias Makoba alisema, agizo hilo lilitolewa baada ya mkutano kati ya waziri mkuu Kassim Majaliwa na viongozi wa vyama vya wafanyabiashara.

Makoba alisema TRA iliagizwa kusitisha ukaguzi wa risiti za kielektroniki kwa ajili ya ukusanyaji kodi, na kuacha kukusanya kodi kwa nguvu.

Wafanyabiashara katika mikoa minane Jumatatu walifunga maduka yao na kufanya mgomo kutokana na mrundikano wa kodi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha