99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Mashirika ya kibinadamu ya UN?na washirika wao wapanua opresheni za msaada huko Darfur na Khartoum nchini Sudan

(CRI Online) Juni 27, 2024

Mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (UN) Jumatano yalisema wao pamoja na washirika wao wanajitahidi kupanua operesheni za msaada huko Darfur na Khartoum nchini Sudan, haswa katika El Fasher, mji mkuu wa jimbo la Darfur Kaskazini.

Shirika la Kuratibu Misaada ya Kibinadamu la Umoja wa Mataifa (OCHA) limesema hali ya El Fasher na sehemu zake za karibu zinaleta wasiwasi mkubwa.

Kwa mujibu wa Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF), watoto zaidi ya 400 wameripotiwa kuuawa au kujeruhiwa vibaya kwenye mapambano ya hivi karibuni.

Limesema, muendelezo wa matumizi ya silaha za mlipuko kwenye maeneo yenye watu wengi umeleta hatari zaidi kwa raia na watu wanaotoa msaada.

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limeripoti kuwa linasambaza msaada wa dharura wa chakula na lishe kwa watu zaidi ya 135,000 katika jimbo la Al-Jazirah nchini humo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha