99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

ANC yasema vyama 10 vya kisiasa vitajiunga na serikali ya umoja wa kitaifa ya Afrika Kusini

(CRI Online) Juni 24, 2024

Chama tawala cha Afrika Kusini, African National Congress (ANC) kimetangaza kuwa vyama 10 vya kisiasa vyenye viti kwenye bunge vimekubali kujiunga na serikali ya umoja wa kitaifa ya Afrika Kusini (GNU) inayoongozwa na ANC.

ANC Jumamosi ilisema baada ya mazungumzo ya wiki mbili, vyama 10 kati ya vyama 18 vyenye viti bungeni vimesaini Taarifa ya Kuridhia ya GNU, vikionesha utayari wao wa kushirikiana, na kuwapa kipaumbele watu wa Afrika Kusini.

Kwa mujibu wa ANC, vyama hivi vimekubali kufuata kanuni za kimsingi zilizomo kwenye Taarifa ya Kuridhia na kufanya juhudi pamoja katika kutimiza malengo yake. ANC imeongeza kuwa milango yake bado iko wazi kwa vyama vingine ambavyo bado havijajiunga na GNU.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha