99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Wataalamu wa kigeni kusaidia kuchunguza ajali ya ndege ya Malawi

(CRI Online) Juni 18, 2024

Rais Lazarus Chakwera wa Malawi ametangaza siku ya Jumapili kwamba serikali ya Malawi itaalika wataalamu wa kigeni kusaidia kuchunguza chanzo cha ajali ya ndege iliyosababisha kifo cha makamu rais wa nchi hiyo Bw. Saulos Chilima na maofisa wengine.

Akiongea kwenye mazishi ya kitaifa, Rais Chakwera amesema wataalam wenyeji wanaendelea na uchunguzi, na kusisitiza umuhimu wa uchunguzi wa kina ili kutoa majibu yanayaowasumbua watu wa Malawi na yeye mwenyewe.

Serikali imetoa wito wa kuomboleza kwa amani huku kukiwa na baadhi ya dalili za mvutano kufuatia nadharia za njama zinazoenea juu ya ajali hiyo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha