99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Makamu Rais wa Malawi athibitishwa kufariki katika ajali ya ndege

(CRI Online) Juni 12, 2024

Rais wa Malawi Lazarus Chakwera amethibitisha kuwa, makamu wake Dr. Saulos Chilima na watu wengine tisa waliokuwa katika ndege ya kijeshi wamefariki baada ya ndege hiyo kupotea Jumatatu asubuhi.

Rais Chakwera amesema katika hotuba yake kwa njia ya televisheni kuwa, timu ya uokoaji iligundua mabaki ya ndege hiyo karibu na mlima ndani ya msitu wa Chikangawa, na kwamba watu wote waliokuwa ndani ya ndege hiyo wamefariki papo hapo baada ya ndege hiyo kuanguka.

Dr. Chilima alikuwa anakwenda kuhudhuria mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Sheria wa nchi hiyo Ralph Kasambara ambaye alikutwa amefariki katika makazi yake huko Lilongwe, mji mkuu wa Malawi, Ijumaa iliyopita.

Kutokana na hali mbaya ya hewa, ndege hiyo ilikuwa inaelekea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kamuzu mjini Lilongwe kabla ya kutoweka kwenye rada.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha