

Lugha Nyingine
Wataalamu wakutana nchini Kenya kujadili sera za kodi barani Afrika
Wataalamu wanakutana Nairobi, Kenya kuanzia siku ya Jumatano kujadili mikakati ya kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani kupitia hatua madhubuti za kodi barani Afrika.
Mkutano huo wa 9 wa Kodi Afrika wa mwaka 2024 ambao utafanyika kwa siku tatu umeleta pamoja ujumbe wa watu zaidi ya 200, wakiwemo wasimamizi wa kodi wa Afrika na washirika wa maendeleo, kushughulikia masuala muhimu ya kodi kama vile mapato kutokana na biashara za kuvuka mipaka.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato ya Kenya, Humphrey Wattanga Mulongo, ametoa wito kwa nchi za Afrika kufanya usimamizi wa kodi na ukusanyaji wa mapato kuwa wa kisasa licha ya kukabiliwa na changamoto kama vile uzembe, ukosefu wa uongozi mzuri na mtiririko haramu wa fedha.
Pia ametoa wito kwa wasimamizi wa kodi wa Afrika kulinda haki za walipa kodi, kuzingatia uadilifu, haki, na uwajibikaji wakati wa kuhudumia wateja, na kufanya mifumo madhubuti ya utatuzi wa migogoro kufikiwa kwa urahisi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma