Timu ya matibabu ya China na shirika la hisani waleta furaha kwa watoto wa Zimbabwe
Kundi la 21 la Timu ya Madaktari wa China nchini Zimbabwe kwa kushirikiana na shirika la hisani la Chinese Loving Mum, wameandaa shughuli maalum ya watoto mjini Harare, kabla ya ujio wa Siku ya Kimataifa ya Watoto.
Shughuli hiyo iliyofanyika katika Nyumba ya Watoto ya Hossana Love in Africa iliyoko kwenye kitongoji cha kaskazini cha Harare, imeleta furaha kwa watoto wa shule ya msingi, ambao wameweza kushiriki kwenye michezo mbalimbali ikiwemo kujifunza aina moja ya mazoezi ya viungo ya kichina iitwayo “Baduanjin”.
Madaktari wa China pia walitumia fursa hii kuonesha mbinu za huduma ya kwanza kwa watoto, ambao waliitikia kwa shauku.
Kiongozi wa timu hiyo ya madaktari wa China, Tan Jianlong amesema, shughuli hiyo imelenga kutoa huduma za afya kwa wenyeji na kuboresha uwezo wa wafanyakazi wa afya wa huko wa kutambua na kutibu magonjwa mbalimbali.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma