Watu zaidi milioni 74 wakabiliwa na hali ya ukosefu wa usalama wa chakula katika pembe ya Afrika
Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa siku ya Jumatano na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) na Mamlaka ya Kiserikali kwa ajili ya Maendeleo ya Afrika Mashariki (IGAD), watu takriban milioni 74.9 katika eneo la Pembe ya Afrika wanakabiliwa na hali ya ukosefu mkubwa wa usalama wa chakula na wanahitaji msaada wa haraka wa kibinadamu.
Ripoti hiyo imesema kati ya idadi hiyo, watu milioni 46.8 wanatoka nchi saba kati ya nchi nane wanachama wa IGAD zikiwemo Djibouti, Kenya, Somalia, Sudan Kusini, Tanzania, Sudan na Uganda, na nyingine ni Burundi, Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Ripoti hiyo imesema kuwa kuongezeka kwa idadi ya watu wenye hali ya ukosefu wa usalama wa chakula katika eneo hilo kutoka watu milioni 58.1 mwezi Februari hadi sasa kumetokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma