99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Kenya na China kuimarisha ushirikiano wa kibiashara wakati?ambapo?uhusiano kati ya China na Afrika unaongezeka

(CRI Online) Mei 29, 2024

Wakati uhusiano wa kibiashara kati ya Kenya na China ukiendelea kupanuka, Kenya iliandaa mkutano wa kiuchumi na kibiashara siku ya Jumatatu mjini Nairobi na kushirikisha wajumbe wa ngazi ya juu kutoka mji wa Shenzhen nchini China.

Mkutano huo pia ulivutia wawakilishi wa kampuni karibu 100 za biashara za ndani na wawakilishi wa China wanaoishi ng'ambo kutoka Shirikisho la Wafanyabiashara wa Kenya.

Rais wa Shirikisho la Kitaifa la Wafanyabiashara na wenye Viwanda la Kenya, Eric Ruto, amesema kampuni za ndani zina shauku ya kushirikiana na viwanda vya utengenezaji bidhaa vya Shenzhen kutokana na teknolojia yao ya hali ya juu katika sekta zinazopewa kipaumbele nchini Kenya, hasa katika nyanja za matibabu, elektroniki na nishati mbadala.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Bao'an huko Shenzhen, Wang Lide, amesema wilaya yake imetengeneza faida linganishi katika bidhaa za matumizi za kielektroniki, vifaa vya nishati mpya, bidhaa za kuzalisha na kuhisi mwanga, vifaa vya kielektroniki, vifaa vya umeme vya semiconductor, mashine za kuchomelea za ultrasonic, na vifaa vya matibabu.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha