

Lugha Nyingine
Tanzania yashinda Mashindano ya TEHAMA China
Vijana watatu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) nchini Tanzania Ndaki ya Teknolojia za Habari na Mawasiliano (TEHAMA), wameibuka washindi katika mashindano ya TEHAMA duniani ya Huawei yaliyofanyika kuanzia tarehe 23 hadi 26 mwezi huu huko Shenzhen, China.
Vijana hao Dickson Mram, Matimu Mahimbo na James Amos ambao wana ujuzi katika uhandisi wa kompyuta, TEHAMA na mawasiliano ya simu, walishiriki katika mashindano hayo yaliyoshindanisha wanafunzi zaidi ya 470 kutoka nchi 49 duniani.
Kufuatia ushindi huo, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari nchini Tanzania, Nape Nnauye, amewapongeza kwa kueleza kuwa ushindi huo unaonesha uwezo uliopo miongoni mwa vijana wa Tanzania katika fani muhimu za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma