

Lugha Nyingine
Wataalamu wakutana Kenya kujadili njia za kukabiliana na dharura za ukame katika Afrika Mashariki
Wataalamu wameanza mkutano wao siku ya Jumanne huko Nairobi nchini Kenya ili kujadili njia za kukabiliana na dharura za ukame katika eneo la Afrika Mashariki.
Mkutano huo wa siku mbili unahudhuriwa na wadau 150 kutoka Mamlaka ya Kiserikali kwa ajili ya Maendeleo ya Nchi za Afrika Mashariki (IGAD), ili kuimarisha ushirikiano katika kuboresha uwezo wa kukabiliana na maafa ya ukame katika ardhi kame na nusu kame.
Naibu Katibu Mtendaji wa IGAD, Mohamed Ware, amesema kuwa watu wa jamii za mpakani, wengi wao ni wafugaji na wakulima, ambao wanategemea mvua zinazoendelea kutokuwa na uhakika. Kutokana na kukosekana kwa miundombinu katika maeneo ya mpakani, juhudi za kibinadamu na misaada mara nyingi inakuwa michache na inachelewa mno kwa waathirika.
Ametoa wito kwa eneo hilo kutekeleza mifumo thabiti ya tahadhari za mapema ili kuboresha uwezo wa kutabiri na kukabiliana na majanga ya ukame.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma