99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

WFP yahitaji dola za kimarekani milioni 109 kushughulikia operesheni za wakimbizi nchini Uganda

(CRI Online) Mei 29, 2024

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani la Umoja wa Mataifa (WFP) limesema linahitaji dola za kimarekani milioni 109 kwa mwaka huu ili kusaidia shughuli za wakimbizi nchini Uganda kwa mwaka huu.

Mkurugenzi wa WFP kanda ya Afrika Mashariki Michael Dunford ambaye yuko ziarani nchini Uganda, amesema mgogoro nchini Sudan umesababisha wakimbizi zaidi ya 33,000 kukimbilia nchini Uganda, huku wengi wao wakiwa wamepoteza mali zao.

Ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kulisaidia Shirika hilo kukabiliana na mgogoro wa Sudan, na kuongeza kuwa, michango mipya ni muhimu ili kuhakikisha wanaendelea kutoa msaada unaohitajika kwa wale wanaohitaji.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha