99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Mjumbe wa China asifu uhusiano usiovunjika na Zambia

(CRI Online) Mei 28, 2024

Konsuli wa uchumi na biashara katika Ubalozi wa China nchini Zambia Bw. Liu Guoyu amesifu ushirikiano usiovunjika kati ya China na Zambia katika miaka iliyopita na kueleza imani yake kuwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili utaendelea kukua katika siku zijazo.

Akiongea kwenye hafla ya kuzindua mradi wa maboresho ya barabara inayoelekea Hospitali ya Mafunzo ya Chuo Kikuu cha Levy Mwanawasa iliyojengwa kwa ufadhili wa China mjini Lusaka, Bw. Liu Guoyu amesema, China itaendelea kuiunga mkono Zambia kwa kuhimiza ujenzi wa mambo ya kisasa, kuboresha maisha ya Wazambia na kutimiza maendeleo na ustawi wa pamoja.

Mradi huo wa barabara iliyopewa jina jipya la Barabara ya Urafiki kati ya Zambia na China, umefadhiliwa na Shirikisho la Wachina nchini Zambia.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha