99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Reli iliyojengwa na China yaongeza biashara ya Ethiopia ya?kuuza na kuagiza bidhaa nje

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 23, 2024

Dereva wa treni wa Ethiopia akipokea daftari dogo kutoka kwa mtangulizi wake Mchina kwenye Stesheni ya Reli ya Adama, Ethiopia, Septemba 9, 2023. (Xinhua/Wang Guansen)

Dereva wa treni wa Ethiopia akipokea daftari dogo kutoka kwa mtangulizi wake Mchina kwenye Stesheni ya Reli ya Adama, Ethiopia, Septemba 9, 2023. (Xinhua/Wang Guansen)

ADDIS ABABA - Reli ya Ethiopia-Djibouti iliyojengwa na China imepunguza kwa kiasi kikubwa muda wa uchukuzi na gharama, na hivyo kuongeza biashara ya uagizaji na uuzaji nje ya Ethiopia, kwa mujibu wa Kampuni ya Ubia ya Reli ya SGR ya Ethiopia-Djibouti (EDR).

Abdi Zenebe, ofisa mtendaji mkuu wa EDR, amesema reli hiyo yenye urefu wa kilomita 752 inakuwa kwa kasi njia inayopendelewa na Ethiopia kwa uagizaji na uuzaji nje wa bidhaa, kama ilivyoripotiwa na Shirika la Habari la Serikali ya Ethiopia siku ya Jumanne. Hivi sasa, asilimia zaidi ya 15 ya jumla ya biashara ya kuagiza na kuuza nje bidhaa ya Ethiopia hufanywa kupitia reli hii.

Zenebe amesema reli hiyo ina ufanisi hasa katika kurahisisha usafirishaji wa bidhaa kuu za Ethiopia zinazouzwa nje ya nchi, kama vile kahawa. Amebainisha kuwa asilimia 98 ya mauzo yote ya nje ya kahawa ya Ethiopia, sasa yanapitia reli hiyo ya Ethiopia-Djibouti.

Takwimu mpya kutoka Mamlaka ya Kahawa na Chai ya Ethiopia zinaonyesha kuwa Ethiopia ilisafirisha kahawa yenye uzito wa tani 174,596 kwenye soko la kimataifa katika kipindi cha miezi tisa ya mwaka huu wa fedha wa Ethiopia (2023/2024), ulioanza Julai 8, ikizalisha mapato ya dola za Kimarekani zaidi ya milioni 835.

Zenebe pia amesema kuwa reli hiyo hivi karibuni itaanza kusafirisha bidhaa za madini, hasa makaa ya mawe na saruji.

Takwimu rasmi zinaonyesha kuwa katika kipindi cha miaka sita iliyopita reli hiyo imesafirisha abiria 680,000 na mizigo yenye uzito wa tani milioni 9.5, huku ikiwa na wastani wa ongezeko la asilimia 39 la mapato ya usafirishaji ya kila mwaka. Tangu Mwaka 2018, reli hiyo imeendelea kuendeleza soko lake la mizigo na kupanua huduma zake, pamoja na huduma za kiwango cha juu kama vile usafirishaji wa bidhaa zinazohifadhiwa baridi, treni za abiria kwa wanavijiji, na treni maalum za usafirishaji wa magari, miongoni mwa nyingine.

Picha hii iliyopigwa tarehe 1 Julai 2023, ikionyesha kahawa yakiwa kwenye Kampuni ya Uuzaji Nje Kahawa ya Mullege, ambayo ni mojawapo ya kampuni za Ethiopia zinazouza kahawa nje, mjini Addis Ababa, Ethiopia. (Xinhua/Michael Tewelde)

Picha hii iliyopigwa tarehe 1 Julai 2023, ikionyesha kahawa yakiwa kwenye Kampuni ya Uuzaji Nje Kahawa ya Mullege, ambayo ni mojawapo ya kampuni za Ethiopia zinazouza kahawa nje, mjini Addis Ababa, Ethiopia. (Xinhua/Michael Tewelde)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha