Shirikisho?la Wafanyabiashara wa China nchini Tanzania lakarabati shule, kutoa vifaa vya michezo
Chen Mingjian, Balozi wa China nchini Tanzania, akizungumza na wanafunzi wa Tanzania kwenye Shule ya Msingi ya Urafiki wa China na Afrika jijini Dar es Salaam, Tanzania, Mei 20, 2024. (Xinhua/Emmanuel Herman)
DAR ES SALAAM – Shirikisho la Wafanyabiashara wa China nchini Tanzania (CEAT) limekabidhi kuta na milango iliyokarabatiwa na kutoa vifaa vya muziki na michezo siku ya Jumatatu kwa Shule ya Msingi ya Urafiki wa China na Afrika iliyopo mji wa bandari wa Dar es Salaam, Tanzania.
Chen Mingjian, Balozi wa China nchini Tanzania, na Kitila Mkumbo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji wa Tanzania, walihudhuria hafla ya makabidhiano ya vitu hivyo.
Mkumbo ameishukuru CEAT kwa msaada huo, akisema elimu bado ni kipaumbele katika mkakati wa nchi hiyo. Amesema msaada huo utaiwezesha shule hiyo yenye wanafunzi 310 kuboresha ufaulu wake.
Mkuu wa Chuo cha Elimu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ilipo Shule ya Msingi ya Urafiki wa China na Afrika, Eugenia Kafanabo amesema shule hiyo imejengwa kwa msaada wa Ubalozi wa China nchini Tanzania chini ya urafiki wa muda mrefu kati ya Tanzania na China.
Balozi Chen ameishukuru CEAT kwa msaada huo utakaowezesha wanafunzi hao kusoma katika mazingira mazuri zaidi na ameongeza kusema kuwa, serikali ya China siku zote inafanya juhudi za kuunga mkono kazi ya kuwaandaa vipaji na kupata maendeleo ya elimu nchini Tanzania.
Amesema shule hiyo ambayo ni miongoni mwa shule 100 za msingi barani Afrika zinazosaidiwa na China chini ya mfumo wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika, imesaidia kuwaandaa watoto kizazi hadi kizazi, na hii imeonesha urafiki kati ya China, Tanzania na Afrika.
Florence Karara, mwalimu mkuu wa shule hiyo, amesema msaada huo utasaidia wanafunzi kusoma na kufanya mazoezi, na hatimaye kuongeza ujuzi na kupata ustadi wa kazi ya ufundi.
Wanafunzi wa Tanzania wakisikiliza wakati Balozi wa China nchini Tanzania Chen Mingjian akizungumza nao katika Shule ya Msingi ya Urafiki wa China na Africa jijini Dar es Salaam, Tanzania, Mei 20, 2024. (Xinhua/Emmanuel Herman)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma