

Lugha Nyingine
Mahakama ya juu nchini Afrika Kusini yatoa hukumu kwamba rais wa zamani Zuma hana hadhi ya?kugombea kwenye uchaguzi ujao
Jacob Zuma akihudhuria kampeni ya Chama cha Umkhonto weSizwe (MK) mjini Johannesburg, Afrika Kusini, Mei 18, 2024. (Picha na Ihsaan Haffejee/Xinhua)
JOHANNESBURG - Mahakama ya Katiba ya Afrika Kusini, ambayo ni Mahakama ya Juu zaidi nchini humo, imetoa hukumu siku ya Jumatatu kuwa rais wa zamani Jacob Zuma hana hadhi ya kugombea ubunge katika uchaguzi ujao ambapo uamuzi huo wa mahakama umekuja kufuatia Tume Huru ya Uchaguzi ya nchi hiyo kuikatia rufaa amri ya Mahakama ya Uchaguzi iliyomruhusu Zuma kubakia kwenye orodha ya wagombea waliopendekezwa na Chama cha Umkhonto weSizwe (MK).
"Zuma alihukumiwa kifungo cha miezi zaidi ya 12... na kwa hiyo hastahili kuwa mgombea na hajatimiza vigezo vinavyotakiwa vya kugombea katika Bunge la Taifa," Mahakama hiyo ya Katiba imesema katika hukumu yake.
Amri ya Mahakama ya Uchaguzi imewekwa kando na maombi ya kupinga yaliyotolewa na Zuma na Chama cha MK yametupiliwa mbali, kwa mujibu wa hukumu hiyo.
Zuma, ambaye alihukumiwa kifungo cha miezi 15 jela kwa kudharau mahakama Mwaka 2021, aliteuliwa kuwa mgombea wa uchaguzi na Chama cha MK.
Afrika Kusini imepanga kufanya uchaguzi wake wa taifa na wa serikali za mitaa Mei 29.
Jacob Zuma akihudhuria kampeni ya Chama cha Umkhonto weSizwe (MK) mjini Johannesburg, Afrika Kusini, Mei 18, 2024. (Picha na Ihsaan Haffejee/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma