99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Shirika la ndege la Ethiopia lazindua kituo cha abiria kilichojengwa na kampuni ya China, na kuongeza uwezo wa kupokea abiria mara dufu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 20, 2024

Watu wakifanya ukaguzi wa tiketi kwenye kituo kipya cha abiria wa ndani katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole mjini Addis Ababa, Ethiopia, Mei 18, 2024. (Xinhua/Michael Tewelde)

Watu wakifanya ukaguzi wa tiketi kwenye kituo kipya cha abiria wa ndani katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole mjini Addis Ababa, Ethiopia, Mei 18, 2024. (Xinhua/Michael Tewelde)

ADDIS ABABA - Shirika la ndege la Ethiopia Ethiopian Airlines, ambalo ni shirika la ndege kubwa na linalokuwa kwa kasi zaidi barani Afrika, limezindua kituo cha abiria wa ndani kilichojengwa na kampuni ya China katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa siku ya Jumamosi.

Mradi huo mpya uliozinduliwa wa kituo cha abiria wa ndani cha shirika hilo la ndege la serikali ya Ethiopia wenye thamani ya dola milioni 50 za Kimarekani katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole, ambao unajumuisha kazi kubwa za upanuzi na ukarabati, unatarajiwa kuongeza kwa zaidi ya mara mbili uwezo wa kupitisha abiria wa kila mwaka wa kituo hicho.

Mesfin Tassew, ofisa mtendaji mkuu (Mkurugenzi Mtendaji) wa Shirika la Ndege la Ethiopia, amesema kwenye hafla hiyo kwamba kituo hicho, ambacho kinaunganisha mji mkuu wa Ethiopia na vituo zaidi ya 20 vya ndani katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki, kinatumika kama kituo muhimu cha kuwezesha mafungamano, maendeleo ya kijamii na kiuchumi, na kukuza sekta ya utalii ya nchi hiyo.

Amebainisha kuwa katikati ya mahitaji yanayokua kwa kasi ya huduma za usafiri wa anga wa ndani na maendeleo ya hivi karibuni katika sekta ya utalii nchini, kituo hicho kimetakiwa kufanyiwa upanuzi mkubwa na ukarabati ili kukidhi mahitaji yanayoongezeka.

Amebainisha kuwa kituo hicho kipya, kilichojengwa na Kampuni ya Ujenzi wa Mawasiliano ya China (CCCC), si tu kwamba kitaongeza uwezo wa shirika hilo kushughulikia wasafiri wengi zaidi bali pia kitaongeza kwa ujumla hali ya usafiri abiria hadi kufikia kiwango cha kimataifa cha huduma ya usafiri wa anga wa ndani.

Waziri wa Utalii wa Ethiopia Nasise Chali amesema jengo hilo la abiria wa ndani lililokarabatiwa na kupanuliwa litakuwa na mchango muhimu katika kurahisisha sekta ya utalii nchini humo kwa kutoa hali bora ya usafiri kwa wasafiri na watalii wa ndani na nje ya nchi, huku pia likiboresha sura ya nchi.

Picha hii iliyopigwa Mei 18, 2024 ikionyesha sehemu ya ndani ya kituo kipya cha abiria wa ndani katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole mjini Addis Ababa, Ethiopia, Mei 18, 2024. (Xinhua/Michael Tewelde)

Picha hii iliyopigwa Mei 18, 2024 ikionyesha sehemu ya ndani ya kituo kipya cha abiria wa ndani katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole mjini Addis Ababa, Ethiopia, Mei 18, 2024. (Xinhua/Michael Tewelde)

Watu wakifanya ukaguzi wa tiketi kwenye kituo kipya cha abiria wa ndani katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole mjini Addis Ababa, Ethiopia, Mei 18, 2024. (Xinhua/Michael Tewelde)

Watu wakifanya ukaguzi wa tiketi kwenye kituo kipya cha abiria wa ndani katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole mjini Addis Ababa, Ethiopia, Mei 18, 2024. (Xinhua/Michael Tewelde)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha