99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Wataalam wasema uhimilivu wa Tabianchi katika Pembe ya Afrika unategemea mifumo thabiti ya tahadhari ya mapema

(CRI Online) Mei 17, 2024

Nchi katika eneo kubwa la Pembe ya Afrika zinapaswa kuwekeza katika mifumo thabiti ya tahadhari ya mapema ili kuongeza uhimilivu wa jamii zilizoko kwenye msukosuko wa mabadiliko ya tabianchi.

Hayo yamesemwa na wataalam kwenye kongamano la mtandaoni lililofanyika jana Alhamisi mjini Nairobi, Kenya.

Philip Omondi, mtaalamu wa mabadiliko ya tabianchi katika Kituo cha Utabiri na Usimamizi wa Hali ya Hewa (ICPAC) kinachohusiana na Mamlaka ya Kiserikali ya Maendeleo kwa Nchi za Afrika Mashariki, amesema eneo hilo linahitaji hatua zenye matarajio zinazotokana na data ili kudhibiti dharura za tabianchi, zikiwemo ukame, mafuriko, vimbunga na moto wa msituni.

Kongamano hilo, lililoandaliwa na ICPAC na washirika wake, lililenga kuangazia jukumu muhimu la mifumo madhubuti ya tahadhari ya mapema katika kuimarisha mwitikio wa hali tabianchi katika eneo kubwa la Pembe ya Afrika.

Naye Mratibu anayeshughulikia uhimilivu wa tabianchi katika Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu (IFRC), Phoebe Wafubwa Shikuku, amesema kuwekeza katika tahadhari za mapema kutasaidia serikali za eneo hilo kuweka mipango ya dharura pindi janga la tabianchi litakapotokea.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha