Serikali ya Tanzania kuongeza vituo vinavyotoa mionzi kwa wagonjwa wa saratani
Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya inaendelea na taratibu za uwekezaji wa kuongeza vituo vingine vinne vya kutibu wagonjwa wa Saratani kwa njia ya mionzi kupitia kujenga majengo na kuwezesha vifaa vitakavyotumika kwa huduma hiyo.
Hayo yamesemwa hivi karibuni na Waziri wa Afya wa nchi hiyo, Ummy Mwalimu kwenye mkutano wa Bunge la nchi hiyo unaoendelea mjini Dodoma.
Waziri Ummy amesema, kwa sasa serikali ina jumla ya vituo vinne ambavyo vinatoa huduma ya matibabu ya saratani kwa njia ya mionzi nchini humo, ambavyo ni Taasisi ya Saratani Ocean Road, Hospitali ya Kanda Bugando, Hospitali binafsi ya Besta na Hospitali ya Good Sammaritan ya Ifakara.
Amesema serikali inaendelea na taratibu za uwekezaji kwa kuongeza vituo vingine vinne vya kutoa tiba hiyo katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, KCMC, Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya na Hospitali binafsi ya Agakhan kwa Tanzania bara, na Hospitali ya Binguni Visiwani Zanzibar.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma