

Lugha Nyingine
Mji wa Chongqing, China warejesha na kuzindua njia za kimataifa za usafiri wa ndege huku kukiwa na wasafiri wengi katika majira ya joto
![]() |
Picha hii iliyopigwa Aprili 1, 2023 ikionyesha mandhari ya pwani ya Chaotianmen, mji wa Chongqing, Kusini Magharibi mwa China. (Xinhua/Tang Yi) |
CHONGQING - Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Chongqing Jiangbei ulio katika mji wa Chongqing, Kusini-Magharibi mwa China utaongeza au kurejesha njia kadhaa za kimataifa wakati wasafiri wako wengi katika majira ya joto.
Kipindi chenye watu wengi kusafiri katika majira ya joto ya mwaka huu zilianza Julai 1 na zitaendelea hadi Agosti 31.
Ili kukidhi mahitaji ya usafiri ya watalii wa ndani na wa kimataifa, Shirika la Ndege la Chongqing limeanza tena safari za ndege za moja kwa moja kati ya Chongqing na Kisiwa cha Phuket nchini Thailand kuanzia Julai 1, na Shirika la Ndege la Xiamen limezindua njia mpya ya usafiri kutoka Chongqing hadi Kuala Lumpur, mji mkuu wa Malaysia. Shirika la Ndege la China litafungua njia mpya kati ya Chongqing na Singapore Julai 23.
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Chongqing Jiangbei unatarajiwa kuhudumia zaidi ya abiria milioni 8 katika majira ya joto, huku ndege za abiria zaidi 55,000 zikipaa na kutua kwenye uwanja huo, ikizidi kiwango kilichorekodiwa katika msimu wa joto wa Mwaka 2019.
Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, idadi ya safari za ndege za abiria za kimataifa na kikanda katika uwanja huo wa ndege imeongezeka kwa kiasi kikubwa. Njia kutoka Chongqing hadi London, Rome, Madrid, Budapest, Dubai, Seoul, Hong Kong na Taipei zimerejeshwa au kufunguliwa.
Kipindi chenye watu wengi kusafiri wakati wa majira ya joto kwa kawaida huwa ni msimu wenye shughuli nyingi kwa huduma za usafiri wa reli na anga za China, kutokana na wanafunzi wa vyuo vikuu kurejea nyumbani na kuongezeka kwa mahitaji ya usafiri kwa ajili ya likizo na safari za kifamilia.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma