99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Msaada wa Marekani nchini Ukraine wafikia dola bilioni 50

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 28, 2023

Shirika la Habari la Interfax-Ukraine limetoa ripoti inayomnukuu Waziri wa Fedha wa Marekani Janet Yellen baada ya mkutano wake na Waziri Mkuu wa Ukraine Denys Shmyhal, kuwa Marekani imetoa msaada unaofikia takriban dola za kimarekani bilioni 50 nchini Ukraine katika nyanja za usalama, uchumi, msaada wa kibinadamu na kijamii tangu kuanza kwa mgogoro kati ya Russia na Ukraine.

Bi. Yellen amebainisha kuwa, Marekani imetoa dola za kimarekani bilioni 14 kusaidia uchumi wa Ukraine kuwa imara zaidi, na inapanga kutenga dola za kimarekani bilioni 8 kwa ajili ya mahitaji kama hayo katika siku za mbele.

Kwa upande wake, Bw. Shmyhal amesema kuwa Mwaka 2022, Marekani ilikuwa mchangiaji mkuu wa fedha katika uchumi wa Ukraine miongoni mwa nchi za kigeni. Kwa mujibu wa makadirio ya serikali ya Ukraine, nchi hiyo inahitaji ufadhili wa dola za kimarekani bilioni 38, ikijumuisha na vyanzo kutoka nje, ili kufidia nakisi ya bajeti mwaka huu.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha