99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Shirika la Afya Duniani (WHO) lasema UVIKO-19 bado ni dharura ya afya

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 31, 2023

Shirika la Afya Duniani (WHO) lasema UVIKO-19 bado ni dharura ya afya

GENEVA - Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema Jumatatu kwamba janga la UVIKO-19 bado linajumuishwa kwenye Dharura ya Afya ya Umma inayofuatiliwa Kimataifa (PHEIC), ambayo inawakilisha kiwango cha juu zaidi cha tahadhari cha WHO.

Tangazo hilo la WHO limekuja huku kukiwa na vifo vya watu vilivyoongezeka na kuripotiwa kila wiki hivi majuzi duniani kote. Baada ya mkutano wake wa tathmini ya robo mwaka kuhusu janga la UVIKO-19 siku ya Ijumaa iliyopita, Kamati ya Dharura ya Kimataifa ya Kanuni za Afya (2005) ya WHO imetangaza jana Jumatatu kwamba UVIKO-19 inaendelea kuwa Dharura ya Afya ya Umma inayofuatiliwa Kimataifa, tangazo ambalo limekubaliwa na Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dk. Tedros Adhanom Ghebreyesus.

UVIKO-19 inabaki kuwa ugonjwa hatari wa kuambukiza wenye uwezo wa kusababisha uharibifu mkubwa kwa mifumo ya afya, kamati hiyo imesema katika taarifa, huku ikikiri kwamba janga la UVIKO-19 linaweza kuwa linakaribia mahali pa kubadilika.

Ingawa maambukizi au chanjo zinaweza kusababisha viwango vya juu vya kinga ya watu duniani na kupunguza athari za ugonjwa mkali na vifo, "kuna shaka kidogo kwamba virusi hivi vitabaki kuwa vimelea vya kudumu kwa wanadamu na wanyama kwa siku zijazo za karibuni," kamati hiyo imesema.

Kisha imetoa wito kwa hatua za muda mrefu za afya ya umma ambazo zitaweka kipaumbele katika kupunguza athari za UVIKO-19 kwa ugonjwa mkali na vifo.

Wakati huo huo, kamati imependekeza kwamba nchi zinapaswa kufikia kiwango cha utoaji wa chanjo kwa asilimia 100 kwa makundi yaliyopewa kipaumbele, kuboresha kuripoti data za uchunguzi wa virusi vya SARS-CoV-2 kwa WHO, na kuhakikisha upatikanaji wa muda mrefu wa hatua za tiba, kama vile chanjo dhidi ya UVIKO-19, uchunguzi na tiba.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha