

Lugha Nyingine
Ushirikiano wa Tabianchi kati ya China na Marekani wasifiwa licha ya matatizo
Picha hii ikionyesha mkutano wa mwisho katika Mkutano wa 27 wa Nchi watia saini (COP27) wa Mkataba wa Mfumo wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (UNFCCC) huko Sharm El-Sheikh, Misri, Novemba 20, 2022. (Xinhua/Sui Xiankai )
NEW YORK – Uwezekano wa ushirikiano wa mabadiliko ya tabianchi kati ya China na Marekani una umuhimu mkubwa kwa Dunia, ingawa vikwazo vipo, waangalizi na wataalam wamesema.
Umoja wa Mataifa unakaribisha mazungumzo ya tabianchi kati ya China na Marekani. Tangazo hilo lilitolewa baada ya kuhitimishwa kwa mkutano kati ya wakuu wa nchi hizo mbili nchini Indonesia Mwezi Novemba, amesema Siddharth Chatterjee, mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini China.
Akizungumza katika mjadala wa jopo hivi majuzi ulioandaliwa na Taasisi ya China nchini Marekani, ambayo ni shirika lisilo la kiserikali la Marekani, Chatterjee amesema mazungumzo ya ngazi ya juu yaliyoanzishwa tena kati ya wajumbe wa tabianchi kutoka nchi hizo mbili "yanaipa Dunia hakikisho na matumaini yanayohitajika zaidi katika nyakati zisizo na uhakika."
Katika Mkutano wa 27 wa Mkutano wa Nchi watia saini (COP27) wa Mkataba wa Mfumo wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi uliofanyika nchini Misri, moja ya matokeo muhimu ni "mazungumzo ya tabianchi kati ya China na Marekani yanarejeshwa," amesema Chatterjee katika hotuba ya video iliyorekodiwa awali.
"Kwa kuweka kando tofauti zao ili kuzingatia mustakabali wa binadamu, ushirikiano wa tabianchi kati ya China na Marekani unaweza kuwa eneo ambalo halitageuka kuwa jangwa tena," amesema Chatterjee.
Mshiriki akitembea kulipita bango kwenye eneo la maonyesho ya mkutano wa 27 wa Mkutano wa Nchi watia saini (COP27) wa Mkataba wa Mfumo wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi huko Sharm El-Sheikh, Misri, Novemba 10, 2022. (Xinhua/Sui Xiankai)
Kuna uwezekano mkubwa wa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, ikiwa ni pamoja na mpito wa ajira katika sekta ya mafuta na maendeleo ya mfumo wa udhibiti na sera za viwango vya mazingira, amesema Chatterjee.
Elizabeth Knup, mwakilishi wa China wa Ford Foundation, amesema kwenye mjadala huo wa jopo hilo kwamba anatiwa moyo na ukweli kwamba mambo yamerejea kwenye njia sahihi.
Ingawa mfumo wa ushirikishaji data na ushirikishaji chini ya Jopo la Kiserikali kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi haujaathiriwa na mvutano kati ya nchi hizo mbili, masomo ya shahada mbili kati ya pande hizo mbili yaliathirika, amesema Xuhui Lee, mkurugenzi wa Kituo cha Uchunguzi wa Dunia cha Yale na mratibu wa programu ya masomo ya shahada mbili kati ya Chuo Kikuu cha Yale na Chuo Kikuu cha Tsinghua cha China.
Teknolojia inaishia kuwa tawi la mzeituni ambalo linaweza kuunganisha nchi hizi mbili na nchi nyingine duniani, amesema Andrew Chung, mwekezaji wa teknolojia na mjasiriamali aliye na uzoefu mzuri wa kuwekeza katika teknolojia ya tabianchi na afya.
"Ni teknolojia ya hali ya juu ambayo itasababisha pande zote mbili kutafuta njia fulani ya kushirikiana ili kufanya teknolojia hizi kibiashara," Chung amesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma